Uncategorized

SIMBA YATAJA KILICHOWAPONZA KUSHINDWA KUTWAA MAPINDUZI, WAJA NA OMBI HILI

admin January 14, 2020 1:57 pm


JOHN Bocco, nahodha wa timu ya Simba amesema kuwa haikuwa bahati yao kushinda kombe la Mapinduzi mbele ya Mtibwa Sugar.

Simba ilitinga hatua ya fainali kwa kuwatoa mabingwa watetezi Azam FC kwa njia ya penalti 3-2, ilifungwa na Mtibwa Sugar jana, Januari 13 bao 1-0.

“Tunamshukuru Mungu tumemaliza mchezo wetu salama, ila haikuwa bahati yetu kutwaa kombe kwani tulipambana na bahati haikuwa kwetu, tunawaomba mashabiki watupe sapoti kwenye mechi zetu zinazofuata.

“Kwa sasa mpango na nguvu kubwa nakuwa kwenye ligi na mechi nyingine tutafanya vema, pongezi nyingi kwa Mtibwa Sugar,” amesema.

KAGERA SUGAR: TUTAPAMBANA KESHO KUPATA POINTI TATU ZA YANGA KUMBE! SARE YA KUFUNGANA MABAO 2-2 INAWAUMIZA YANGA, MILIONI 150 ZILIZOYEYUKA ZINAWAUMA KINOMA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply