Uncategorized

BEKI YANGA ATAKA KURUDI KMC, AGOMEA TIMU NYINGINE JUMLA

admin January 27, 2020 2:13 pm


ALLY Ally, beki wa Yanga amesema kuwa yupo tayari kuibukia kwenye Klabu yake ya zamani KMC  kwa mkopo na sio kwenda kwenye timu nyingine ikishindikana atabaki Yanga.

Ally alijiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha kubwa kwa kandarasi miaka miwili akitokea KMC, kwa sasa uongozi wa Yanga umepanga kumtoka kwa mkop kwenda JKT Tanzania jambo ambalo ameligomea.

“Sipo tayari kwenda kwenye timu nyingine kwa sasa, labda nirudi KMC hapo nipo tayari ila sehemu nyingine hapana siwezi kwenda,” amesema.

Jamila Mutabanzi, Ofisa Habar wa JKT Tanzania aesema kuwa Ally alipaswa ajiunge na wenzake kwenye mazoezi ila bado hajatokea.

“Tulipewa barua na Yanga kwamba wanataka aje kwetu kwa mkopo, suala la yeye kugoma hilo wanapaswa wamalizane ndani ya Yanga,” amesema.

JESHI LA AZAM FC LILIOANZA LEO DHIDI YA FRIENDS RANGERS UWANJA WA UHURU MWENDO MPYA KWA YANGA, LAZIMA EYMAEL AWEKEZE HUKU…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply