Uncategorized

VIRGIL VAN DIJK KUONDOKA LIVERPOOL

admin February 4, 2020 9:39 pm

HUKO ughaibuni, taarifa inayosambaa kwa kasi ni Juventus kujipanga kumng’oa beki wa Liverpool, Virgil van Dijk katika dirisha lijalo la usajili wa majira ya joto barani Ulaya.

Taarifa iliyoandikwa na Gazeti la The Sun la Uingereza jana, ilieleza kuwa Juve wamemtengea beki huyo donge nono la pauni milioni 150, sawa na Sh bilioni 456.

Miamba hiyo ya Serie A inaamini kuwa Mholanzi huyo atakuwa tayari kutafuta changamoto mpya kama timu yake ikibeba ubingwa wa Premier msimu huu na wanataka kumfanya awe beki ghali zaidi duniani kwa mara nyingine tena.

Tangu atue Anfield, Van Dijk ameisaidia Liverpool kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Dunia la Klabu na Uefa Super Cup huku wakiwa mbioni kubeba ubingwa wa kwanza wa Premier baada ya kupita miaka 30.
MCHEZAJI COASTAL UNION ALIVYOWAFANYIA KITU MBAYA SIMBA MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO, LIPO MTAANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply