Uncategorized

YANGA: MORALI YA WACHEZAJI IPO VIZURI, TUTAPAMBANA MBELE YA RUVU

admin February 7, 2020 10:14 am


LUC Eymael, Mkuu wa Yanga amesema kuwa anaamini wachezaji wake watafanya vizuri kwenye mchezo wao wa kesho, Februari 8,2020, dhidi ya Ruvu Shooting utakaochezwa Uwanja wa Uhuru majira ya saa 10:00 jioni.


Eymael amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na kila mchezaji anatimiza majukumu yake mazoezini jambo linalompa nguvu ya kuamini kwamba atapata matokeo mazuri.

“Wachezaji wanaonyesha ari na nia ya kupambana kwa ajili ya timu, ligi ina ushindani mkubwa na kila timu inahitaji matokeo hata sisi pia tunahitaji ushindi,” amesema.

Yanga ikiwa imecheza mechi 17 imepoteza mechi tatu ambapo ya kwanza kupoteza ilikuwa mbele ya Ruvu Shooting kwa kuchapwa bao 1-0 Uwanja wa Uhuru.
PIGO, WACHEZAJI SITA WA SIMBA KUIKOSA JUMLA JKT TANZANIA LEO UHURU KIKOSI CHA SIMBA VS JKT TANZANIA. KICHUYA AANZA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply