Uncategorized

BARCELONA KUFANYA USAJILI MAALUMU KUOKOA JAHAZI, MAJEMBE HAYA YATAJWA

admin February 8, 2020 4:14 am


IMEELEZWA kuwa Klabu ya Barcelona inaweza kufanya usajili maalumu msimu huu ili kuongeza nguvu kwenye kikosi chake.

Kwa sasa kikosi hicho kina wachezaji wawili ambao ni majeruhi watakaokaa nje ya Uwanja muda mrefu.

Ousmane Dembele ameungana na mshambuliaji Luis Suarez kwenye orodha ya majeruhi jambo ambalo limevuruga hesabu ndani ya timu.

Licha ya dirisha la usajili kufungwa bado kanuni zinaruhusu kwa klabu kufanya hivyo endapo kutakuwa na majeruhi watakaovuruga hesabu za timu, ndivyo mambo yalivyo kwa sasa.

Upo uwezekano wa Barcelona kuomba kibali na inaweza kusajili mchezaji yoyote kutoka ndani ya Hispania au yeyote ambaye hana klabu.

Ikiwa mipango itajibu basi Christhian Stuan na William  Sociedad wanapigiwa chapuo kuingia kwenye utawala wa Kocha Mkuu wa Barcelona, Quique Setien. 

SIMBA : WAPINZANI WETU WALIKUWA VIZURI, TULISHINDWA KUTUMIA NAFASI IGHALO: MAMA ALILIA ALIPOSKIA NATUA UNITED, ISHU YA MSHAHARA HAIKUMPA TABU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply