Uncategorized

SAMATTA ATAKA MABAO 14 VILLA

admin February 9, 2020 12:44 pm

MSHAMBULIAJI mpya wa aston Villa, Mtanzania, Mbwana Samatta amepanga kufunga katika kila mchezo wa Ligi Kuu England ‘Premier League’ kwa lengo la kuisaidia timu hiyo isishuke daraja msimu huu. Samatta amepanga kufunga mabao hayo ikiwa tayari ameanza katika mchezo wa kwanza kwenye ligi dhidi ya  Bournemouth ambao Villa ilipoteza kwa mabao 2-1.

Villa ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi 25 huku ikiwa imesaliwa na mechi 13 pekee kumaliza ligi, akifanikiwa kucheza zote, anaweza kufikia idadi hiyo.

Baba mzazi wa mshambuliaji huyo, mzee Ally Samatta alisema kuwa mtoto wake amemuhakikishia anataka kufunga katika kila mchezo kwenye ligi hiyo kwa lengo la kuinusuru timu yake isishuke daraja.

“Kikubwa ambacho amenieleza baada ya kufanikiwa kufunga katika mechi yake ya kwanza kwamba amepanga kufunga katika kila mchezo watakaocheza ili kuinusuru timu ishuke.

“Unajua kwa sasa Aston Villa hawapo kwenye nafasi nzuri wanapambana wasishuke daraja sasa yeye anataka kuitumia nafasi hiyo kuibakisha timu ligi kuu na uzuri hizi kelele zilizopigwa juu ya wachezaji wenzake huenda zikasaidia kwa yeye kufanya makubwa kwenye timu yake,” alisema mzee Samatta.
HARMONIZE AKUSANYA KIJIJI MWANZA, AVUNJA REKODI – VIDEO MMASAI WA YANGA, TUMEMTEKENYA MASAU BWIRE – VIDEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply