Uncategorized

WAWILI WA SIMBA WAACHWA DAR, KUIKOSA MTIBWA SUGAR LEO

admin February 10, 2020 9:17 pm

MZAMIRU Yassin naMiraj Athuman ‘Sheva’ nyota wa Simba wataukosa mchezo wa kesho Februari 11,2020 dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Kwenye jumla ya mabao 42 ambayo Simba imefunga msimu huu ndani ya ligi, wamehusika kwenye jumla ya mabao 10 ambapo Sheva amefunga mabao sita na kutoa pasi moja ya bao huku Mzamiru akitoa jumla ya pasi tatu za mabao.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema kuwa wachezaji wao wawili wameachwa Bongo kutokana na kutokuwa fiti.
“Tutawakosa wachezaji wetu wawili ambao ni Mzamiru Yassin na Miraj Athuman hawa wamebaki Bongo kwa kuwa bado hawajawa fiti ila maendeleo yao yapo vizuri,” alisema Rweyemamu.
Mzamiru mara ya mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa kwenye Januari 4,2020 kwenye mechi dhidi ya Yanga na Sheva mechi yake ya mwisho ilikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar, Januari 13,2020.
KOCHA SIMBA ATANGAZA UBABE KWA MTIBWA – VIDEO HIVI HAPA VIGONGO VITANO VIKALI KWA YANGA FEBRUARI, EYMAEL ATOA NENO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply