Uncategorized

MASHABIKI MAN UNITED SIKIENI HII KUTOKA KWA BOSS WENU

admin February 15, 2020 9:07 pm

Mkurugenzi wa Manchester United, Ed Woodward amesema anaona nafasi ya kikosi chao kufanya vizuri msimu ujao huku akiamini msimu huu wanaweza kutwaa mataji ya Europa na FA.

Hivi karibuni Woodward alivamiwa nyumbani kwake na kundi la mashabiki wa Manchester United waliokuwa wakishinikiza aondoke sababu amekuwa akilegalega kufanya usajili wa wachezaji ndani ya timu hiyo.

“Naona tunaelekea njia nzuri, usajili wa Bruno Fernandes na wachezaji waliopo majeruhi wanarejea taratibu kikosini, ni dalili njema kwetu, uhakika ni mkubwa kufanya vizuri msimu ujao ila msimu huu tunaweza kutwaa Kombe la Europa na FA.

“Tangu Ole Gunnar Solskjaer ameichukua timu anajua kipi cha kufanya, sisi viongozi tunamuunga mkono kwa kila kitu, usajili tuliofanya chini yake umefanikiwa kwa kiasi kikubwa tofauti na misimu iliyopita,” alisema.
MWAKYEMBE AWAONYA WATANZANIA KUHUSIANA NA SAMATTA – VIDEO KOCHA SIMBA AMPOTEZA LUC WA YANGA, REKODI YAANDIKWA – VIDEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply