Uncategorized

SIMBA YAIWAHI KAGERA SUGAR KAMBINI FASTA

admin February 16, 2020 5:22 pm


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo wamerejea kutoka Iringa ambako walikuwa na mchezo wa ligi na Lipuli, Jana Samora.

Simba ilishinda mchezo huo kwa kuifunga Lipuli bao 1-0 lililofungwa na nahodha, Jonh Bocco.

Leo kikosi kimefika Dar es Salaam na kimeingia kambini kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa Jumanne Februari,18 Uwanja wa Taifa.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Kaitaba Simba ilishinda kwa mabao 3-0 ambapo Meddie Kagere alipachika mabao mawili na bao lingine alifunga Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.

Bocco amesema kuwa wanatambua kuwa mechi yao itakuwa ngumu ila watapambana kupata pointi tatu


SPURS SIO WATU WAZURI, WAIBAMIZA ASTON VILLA YA SAMATTA USIKU KWELI YANGA YAIVUTIA KASI POLISI TANZANIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply