Uncategorized

PLISI TANZANIA YATAJA KITAKACHOWAPA POINTI TATU LEO MBELE YA YANGA

admin February 18, 2020 5:22 am


FRANK Lukwaro, Ofisa Habari wa Polisi Tanzania amesema kuwa ni ngumu kwa Yanga leo kuondoka na pointi tatu kutokana na maandalizi makini ya kikosi waliyoyafanya.

Leo Uwanja wa Ushirika Yanga itamenyana na Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ukiwa ni wa mzunguko wa pili.

Lukwaro amesema:”Tupo tayari kupambana mbele ya Yanga, kikosi kimeandaliwa vizuri na wachezaji wana morali kubwa ya kutafuta ushindi, imani yetu tutapata pointi tatu na itakuwa ngumu kwa wapinzani wetu kusepa na pointi tatu endapo tutashinda.

“Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu na kuishangilia ili kuongeza nguvu kwa wachezaji kuonyesha juhudi,”.

Polisi Tanzania ipo nafasi ya nane kwenye msimamo na ina pointi 33 itamenyana na Yanga iliyo nafasi ya tatu na ina pointi 39.

TFF YATOA SABABU YA KILICHOTIBUA LIGI KUU TANZANIA BARA OLE GUNNAR SOLSKAJER AICHAPA CHELSEA MABAO 2-0, LAMPARD ALIA NA VAR

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply