Uncategorized

KMC YAZIACHA POINTI SITA JUMLA NYANDA ZA JUU KUSINI

admin February 23, 2020 5:41 am


TIMU ya KMC imeacha pointi sita jumla ugenini kwenye mechi zake mbili ilizokuwa ikicheza nyanda za juu Kusini.

KMC ilianza kupoteza mbele ya Namungo FC Uwanja wa Majaliwa kwa kufungwa mabao 2-1 kisha ikafuata kupoteza mbele ya Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona kwa kufungwa mabao 2-1.

KMC imekubali kufungwa mabao manne huku wao wakishinda mabao mawili kwenye mechi mbili walizocheza.

Wafungaji wa mabao ya KMC ni James Msuva na Mohamed Samatta.

Kwenye ushindi wa Ndanda SC wa mabao 2-1 mbele ya KMC FC mabao yalifungwa na Kiggi Makasi  dakika ya 2 na Abdulrazack Ramadhan dakika ya 70 na lile la KMC likifungwa na Mohamed Samatta dakika ya 77

SIMBA BAADA YA KUMALIZIANA NA BIASHARA SASA HAO KWA STAND UNITED TAMBO ZA MASAU BWIRE ZAJIBIWA KWA VITENDO NA POLISI TANZANIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply