Uncategorized

WILDER ASEMA VAZI ALILOVAA LILICHANGIA YEYE KUPIGWA NA TYSON FURY

admin February 25, 2020 9:14 am


Bondia Deontay Wilder amesema vazi alilovaa wakati akiingia ulingoni kuzichapa na Tyson Fury raia wa Uingereza, lililichangia yeye kupigwa.

Wilder raia wa Marekani ambaye hakuwa amewahi kupigwa alipoteza pambano lake la kwanza katika raundi ya saba kwa kuchapwa kwa KO baada ya kocha wake kurusha taulo ulingoni.



Wilder amesema kwa muda mwingi alijisikia miguu yake haina nguvu na anaamini uzito wa vazi lile lililokuwa likimuonyesha kama jitu la kutisha lilichangia sana.


“Kuanzia raundi ya pili nilisikia sina nguvu, hakika niliumia sana. Niliona kila kitu hakiwezekani lakini ndio hivyo imepita na ninataka kuanza upya tena,” alisema Wilder.


Tayari Wilder na timu yake wameomba pambano la tatu ambalo litakuwa ni la kumaliza ubishi dhidi ya Fury.

SALAMU HIZI ZATUMWA GWAMBINA FC KUTOKA YANGA WILDER AMFUKUZA KOCHA ALIYETUPA TAULO ULINGONI, KOCHA MKUU AMRUKA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply