Uncategorized

MANCHESTER CITY YABEBA UBINGWA WA CARABAO MBELE YA SAMATTA

admin March 1, 2020 9:48 pm


ASTON Villa timu anayokipiga Mbwana Samatta, jana Machi Mosi imeshuhudia ubingwa ukisepa jumla mpaka mikononi mwa wapinzani wao Manchester City.

Villa iliyo chini ya Dean Smith ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Carabao iliyochezwa Uwanja wa Wembley.

City ilianza kuandika bao la kwanza dakika ya 20 kupitia kwa Arguero na bao la pili dakika ya 30 kupitia kwa Rodri.

Samatta alipachika bao dakika ya 41 kwa kichwa kilichozama nyavuni jumlajumla.

Timu ya mwisho kucheza na City fainali ilikuwa ni Watford na ilichapwa mabao 6-0 na alipocheza na Arsenal 2015 aliichapa 4-0 hivyo Samatta amefanya maajabu maana wengi walidhani ingechapwa mabao saba.

JURGEN KLOPP AIPA TANO WATFORD KWA KUMTIBULIA REKODI YAKE MAZIMA SAMATTA AWEKA REKODI MOJA MATATA SANA, KAMTUNGUA GUARDIOLA HANA HAMU NAYE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply