Uncategorized

SAMATTA AWEKA REKODI MOJA MATATA SANA, KAMTUNGUA GUARDIOLA HANA HAMU NAYE

admin March 1, 2020 9:48 pm


MBWANA Samatta, nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu England leo ameweka rekodi mpya kwa kufunga bao katika mechi ya fainali ya kuwania Kombe dhidi ya kikosi cha Manchester City kinachonolewa na kocha Pep Guardiola.

Mara ya mwisho aliyemfunga bao alikuwa Wayne Rooney katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 2011.

Baada ya hapo, Guardiola akiwa na timu tofauti ameshiriki fainali 8 bila ya timu yake kuruhusu bao hadi Samatta kutoka Tanzania alupoliona tundu na kupachika mbao wake wa kwanza kwenye Fainali iliyochezwa Uwanja wa Wembeley.


City ilianza kuandika bao la kwanza dakika ya 20 kupitia kwa Arguero na bao la pili dakika ya 30 kupitia kwa Rodri.

Bao la Mtanzania Samatta alilipachika dakika ya 41 kwa kichwa matata kilichozama nyavuni jumlajumla.

MANCHESTER CITY YABEBA UBINGWA WA CARABAO MBELE YA SAMATTA VIDEO: YACHEKI MABAO YA KIUNGO WA SIMBA LUIS MIQUISSONE MBELE YA KMC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply