Yanga SC

OKELLO AZUA MJADALA YANGA, MABAO 9 LAKINI HAONI CHA AJABU

Vardo May 23, 2026 10:53 pm

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Allan Okello ameweka wazi kuwa licha ya kuendelea kufunga mabao katika kila mchezo, kwake mafanikio ya kibinafsi si kipaumbele kikubwa, bali lengo kuu ni inavuna alama tatu muhimu kila wanaposhuka dimbani.

Okello ambaye ameendelea kuwa mmoja wa wachezaji muhimu ndani ya kikosi cha Yanga, amekuwa na kiwango bora katika michezo ya hivi karibuni, akiwa na mchango mkubwa wa mabao na pasi za mwisho.

Hadi sasa, tayari amefikisha mabao tisa msimu huu, hali inayoendelea kumfanya kuwa miongoni mwa silaha muhimu za timu hiyo.

Akizungumzia hali yake ya sasa, Okello amesema ushindi wa timu ndio unaopewa uzito zaidi kuliko rekodi binafsi za ufungaji, akisisitiza kuwa mpira wa miguu ni juhudi za pamoja na sio mtu mmoja mmoja.

“Mechi hii imeisha na sasa tunaangalia michezo ijayo ili kupata alama tatu. Si jambo rahisi kufunga mabao mengi katika kila mchezo, lakini muhimu zaidi ni mafanikio ya timu kuliko mafanikio binafsi,” amesema Okello.

Kauli hiyo imekuja mara baada ya mchezo wa hivi karibuni dhidi ya Singida BS uliopigwa katika Uwanja wa KMC Complex, ambapo Okello alikuwa miongoni mwa wachezaji waliotoa mchango mkubwa.

Ameongeza kuwa mafanikio yake ya kufikisha mabao tisa hadi sasa ni matokeo ya kazi ya pamoja ya timu nzima, akisisitiza kuwa bado ana jukumu la kupambana zaidi kuhakikisha Yanga inaendelea kupata matokeo chanya.

“Tunaendelea kupambana, kujitoa kwa kila kitu, na kuhakikisha kila mchezo tunapata alama tatu,” ameongeza.

Yanga sasa inaelekeza nguvu kwenye michezo inayofuata huku ikiwa na malengo ya kuendeleza ushindani mkali katika mbio za ubingwa.

CELTA VIGO KUWANIA NAFASI YA KUSHIRIKI MICHUANO YA ULAYA LEO SIMBA YATIKA KWA HASIRA MECHI YA KISASI DHIDI YA DODOMA JIJI