Uncategorized
SIMBA:MASHABIKI WANATUPA NGUVU YA KUPAMBANA UWANJANI
JOHN Bocco, nahodha wa Simba amesema kuwa wanawashukuru mashabiki kwa sapoti yao kwani inawapa nguvu ya kupata matokeo kwenye mechi wanazocheza ndani ya Ligi Kuu Bara.
Simba jana ilishinda mbele ya KMC mabao 2-0 na kuifanya isepe na pointi tatu kwenye mchezo huo wa kwanza mwezi Machi, Mosi.
Bocco amesema:”Kikubwa ni sapoti ambayo tunapata kutoka kwa mashabiki inatupa nguvu na kutufanya tupambane kupata matokeo, kazi bado inaendelea,” amesema.
Simba imefikisha jumla ya pointi 65 ikiwa kileleni baada ya kucheza mechi 25.
Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.