Simba SC

SIMBA WANATAKA KUSAJILI KIPA MPYA…? UKWELI WOTE HUU HAPA….

admin June 24, 2026 8:15 am

SIMBA imeendelea kusaka kipa bora kila kona ya Afrika miongoni mwa makipa wanaowafuatilia kipa Mgaboni Loyce Mbaba anayekipiga Stella Abidjan ya Ivory Coast.

Huyu anakuwa kipa wa kwanza kutajwa Simba, licha ya kwamba ndani ya kikosi hicho kuna makipa wanaochezea eneo hilo akiwemo Djibrilla Kassali, ambaye mkataba wake unamalazika mwishoni mwa msimu huu.

Si hivyo tu, Simba pia imerusha ndoano yake kwa kipa bora wa Ligi Kuu ya Zimbabwe, Nelson Chadya anayeichezea Scottland FC.

SABABU ZA SIMBA KUSAKA KIPA MPYA

Simba ukiiangalia kwa haraka unaweza kusema haina uhitaji wa kipa mpya kwani wana Kassali anayecheza sasa na Moussa Camara ambaye naye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu ingawa jina lake lilitolewa kwenye mfumo wa usajili dirisha dogo.

Tuanze kwa Kassali, licha ya Simba kuonyesha kiwango kizuri kwenye mechi za hivi karibuni tangu dirisha dogo, lakini uongozi haujaridhishwa kikamilifu na kiwango cha kipa huyo Niger.

Kwa upande wa Moussa Pinpin Camara, licha ya kupona majeraha na kuanza mazoezi, mkataba wake unaomalizika mwishoni mwa msimu huu, lakini Simba haina mpango wa kumwongezea mkataba mpya.

Upande wa wazawa kipa Yakub Suleiman bado anakabiliwa na majeraha ya muda mrefu, huku akitarajiwa kukosa nusu msimu ujao, hali inayomwacha Hussein Abel pekee katika eneo salama.

KINACHOENDELEA

Taarifa zinaeleza kuwa jina la kipa Loyce Mbaba limefika kwenye meza ya mabosi wa usajili wa klabu hiyo huku likiwa sehemu ya mchakato wa kutafuta chaguo sahihi la kuongeza ushindani ndani ya kikosi.

“Simba bado haijafikia hatua ya kufanya uamuzi wa mwisho kwani bado kuna majadiliano ya ndani kuhusu kipa gani atakayepewa nafasi ya kusajiliwa kabla ya maandalizi ya msimu mpya kuanza rasmi.

“Ni kweli jina la Loyce Mbaba limeongezwa kwenye orodha ya makipa wanaotazamwa. Lakini bado hakuna uamuzi wa mwisho uliopitishwa kwa sababu kuna kikao kitafanyika wiki ijayo kujadili kipa atakayechukuliwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya klabu hiyo Crescentius Magori aliwahi kuzungumza na kusema kuwa, Usajili wa kipa wakigeni wa kikosi hicho utafanyika mwisho wa msimu.

WANAOTAJWA

Ukiachana na huyu ambaye uamuzi wake yatafanyiwa kazi wiki ijayo, lakini Simba imetajwa kufuatilia makipa wengine ambao nao ni wa kigeni ambao ni:

Makipa wanaotajwa ni Issa Fofana wa Al Hilal (Sudan) kipa huyu raia wa Ivory Coast, Stanley Nwabali kipa huyu wa timu ya taifa ya Nigeria (Super Eagles) anahusishwa na Simba SC baada ya kuachana na klabu ya Chippa United ya Afrika Kusini kwa makubaliano ya pande zote mbili.

YANGA vs AZAM….USHINDI UPO HAPA LEO…ATAKAYEWAHI KAWAHI…