Yanga SC

AZIZ KI AIBUA GUMZO KUBWA BAADA YA YANGA KUFIKA MEZANI

Vardo June 24, 2026 12:53 pm

UONGOZI wa Yanga umeanza rasmi harakati za kumrudisha kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki kwa kuingia kwenye mazungumzo na klabu yake ya Al Ittihad ya Libya, huku ukilenga kukamilisha usajili huo kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa Yanga imeonyesha dhamira kubwa ya kumrejesha nyota huyo aliyewahi kuwa nguzo muhimu katika kikosi hicho, akichangia mafanikio makubwa ya timu kwenye mashindano ya ndani na kimataifa.

Inaelezwa kuwa mazungumzo kati ya Yanga na Al Ittihad yanaendelea katika mazingira mazuri, jambo linaloongeza matumaini ya kufikiwa kwa makubaliano yatakayomuwezesha Aziz Ki kurejea tena Jangwani.

Vyanzo vya karibu na mchakato huo vimebainisha kuwa hakuna changamoto kubwa inayoweza kuzuia dili hilo kukamilika, huku pande zote zikionekana kuwa na nia ya kuona usajili huo unafanikiwa.

“Aziz Ki aliondoka Yanga akiwa ameacha alama kubwa kutokana na kiwango chake bora, ubunifu wake wa hali ya juu na uwezo wake wa kubadili matokeo katika mechi muhimu. Ndiyo maana bado ana nafasi ya pekee mioyoni mwa mashabiki wa Yanga,” kimesema chanzo hicho.

Iwapo usajili huo utakamilika, utakuwa ni habari njema kwa mashabiki wa Yanga ambao wameendelea kuonyesha hamu ya kumuona kiungo huyo akivaa tena jezi za timu hiyo baada ya kuondoka mwanzoni mwa msimu uliopita.

Aidha, kurejea kwa Aziz Ki kunatajwa kuwa kutaimarisha zaidi kikosi cha Yanga kinachojiandaa kwa ushindani mkali wa Ligi Kuu pamoja na michuano ya kimataifa, huku benchi la ufundi likitarajia kupata chaguo muhimu katika eneo la ushambuliaji.

Nyota huyo yupo hapa nchini kwa ajili ya mapumziko mafupi na hivi karibuni alienda Dodoma kwa ajili ya kurejesha fadhila katika jamiii kwa kutembea watoto yatima na kutoa sadaka.

SIMBA WANATAKA KUSAJILI KIPA MPYA…? UKWELI WOTE HUU HAPA…. MAGEUZI YA SIMBA BARKER KULINDWA APEWA MUDA WA KUJENGA DOLA