Dabi ya Kariakoo FVS
Michezo Bongo

Dabi ya Kariakoo: TFF Yatangaza FVS na Vifaa vya Sumu Vyumbani

Vardo August 11, 2026 9:07 pm

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limethibitisha rasmi kuwa mchezo wa Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga SC na Simba SC utashuhudia mapinduzi makubwa ya kiteknolojia, baada ya kuruhusu matumizi ya usaidizi wa video kwa waamuzi ili kuondoa utata uwanjani.

Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa utapigwa kesho kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, huku TFF ikiweka wazi safu ya waamuzi watakaosimamia sheria uwanjani hapo:

  • Mwamuzi wa Kati: Ahmed Arajiga (Manyara)

  • Msaidizi wa Kwanza: Mohammed Mkono (Tanga)

  • Msaidizi wa Pili: Leonard Mkumbo (Manyara)

Teknolojia ya FVS Kazi Kazi Uwanja wa Amaan

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, waamuzi hao wote watasaidiwa na teknolojia ya Football Video Support (FVS) — mfumo maalum unaofanya kazi sawa na VAR — ili kusaidia kufanya maamuzi sahihi kwenye matukio tata.

Bosi mmoja wa juu kutoka TFF ameeleza kuwa waamuzi waliopangwa tayari wamefanya vizuri kwenye mafunzo maalum yaliyotolewa na wakufunzi wa kimataifa.

“FVS itakuwepo na waamuzi hawa ni miongoni mwa waliofanya vizuri zaidi kwenye mafunzo yaliyoendeshwa na wakufunzi kutoka nje. Wakufunzi wao pia watakuwa wakifuatilia kila kinachoamuliwa uwanjani ili kuhakikisha mechi hii kubwa inaamuliwa kwa haki na usawa,” alisema kiongozi huyo.

Teknolojia hii ya FVS inatarajiwa kuanza kutumika rasmi kwenye michezo mingine ya Ligi Kuu kuanzia msimu ujao.


Mwisho wa Kukimbia Vyumba: Vifaa vya Kupima Sumu Vyatua

Mbali na FVS, TFF kupitia Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imechukua hatua madhubuti kukomesha migogoro ya timu kugomea vyumba vya kubadilishia nguo kwa hofu ya kupuliziwa hewa au dawa zenye sumu.

Vifaa vya kisasa vya kupima ubora na usalama wa hewa vimeshawasili visiwani Zanzibar na vitatumika mara moja endapo timu yoyote itawasilisha wasiwasi kuhusu usalama wa chumba chao.

“Mambo ya timu kukimbia vyumba hayatatokea tena kuanzia mchezo wa kesho. Tumenunua vifaa vya kisasa vinavyotoa majibu ya haraka. Timu ikilalamika tutapima hapo hapo; tukikuta kuna shida tutachukua hatua, na ikionekana hakuna kitu tutawajibu. Wakikaidi, kanuni zitachukua mkondo wake,” alisisitiza bosi huyo.

Adhabu Kali kwa Kakukaidi Kanuni

Ili kulinda taswira ya soka la Bongo, TFF imeweka kanuni kali ambapo timu yoyote itakayokataa au kukimbia kutumia vyumba rasmi vya kubadilishia nguo bila sababisha za msingi itakatwa pointi tano (5) kwenye msimamo wa ligi.

Magori Afunguka Siri ya Simba SC Kuteka Soko la Usajili Swahili