Uncategorized

SIMBA YAZITAKA POINTI TATU ZA SINGIDA UNITED

admin March 10, 2020 9:27 pm


SIMBA leo itakuwa na kazi ya kumenyana na Singida United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Uhuru majira ya saa 10:00 jioni.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Simba ilishinda kwa bao 1-0 lililopachikwa kimiani na Miraj Athuman aliyemalizia pasi ya Mzamiru Yassin.

Uongozi wa Simba umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya kuzisaka pointi tatu baada ya kupoteza mbele ya Yanga mchezo uliopita kwa kufungwa bao 1-0.

Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kuendeleza kutoa burudani na kupata ushindi mbele ya wapinzani wake.

MVUA YATIBUA MIPANGO YA POLISI TANZANIA V MTIBWA SUGAR YANGA KWENYE KIBARUA KINGINE KESHO TAIFA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply