Uncategorized

HIKI NDICHO ANACHOKIFANYA MORRISON KUJILINDA NA CORONA

admin March 21, 2020 5:31 am


BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kwa kipindi hiki cha maambukizi ya Corona anachukua tahadhari kwa kukaa ndani na kuskiliza muziki ili kuwa salama.

Ligi Kuu Bara imesimamishwa na Serikali, Machi 17 na inatarajiwa kurejea Machi 17 iwapo hali ya maambukizi ya Virusi vya Corona yatapungua.

“Kutokana na kusambaa kwa virusi vya Corona na ligi kusimama ninachokifanya kwa sasa ni kuchukua tahadhari ambapo najiepusha na mikusanyiko ya watu pamoja na kujichanganya sehemu ambazo sio salama kwa lengo la kujikinga.

“Nikiwa nyumbani ninapenda kuskiliza muziki na kufanya mazoezi binafsi ili kulinda kipaji changu, kikubwa kwa wakati huu ni kuona kwamba kunakuwa na hali ya utulivu na ile hofu inaondoka,” amesema.



TFF KUWAPIGA STOP WACHEZAJI WATAKAOVUKA MIPAKA YA TANZANIA SIMBA YATOA SOMO HILI KUHUSU CORONA KWA WATANZANIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply