Uncategorized

SIMBA YATOA SOMO HILI KUHUSU CORONA KWA WATANZANIA

admin March 21, 2020 11:31 am

GADIEL Michael, beki wa Simba amewataka watanzania kuchukua tahadhari za kujilinda dhidi ya Corona ili kulinda afya zao na familia kiujumla.

Akizungumza na Saleh Jembe, Gadiel amesema kuwa kwa sasa kinachotakiwa ni kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake.

“Ni muhimu kuchukua tahadhari kwa wakati huu ambao tupo na kila mmoja akiwa mlinzi wa afya ya mwenzake itapunguza kuenenea kwa maambukizi ya Corona.

“Kikubwa ni utulivu kwa watanzania na kuondoa ile hofu ambayo ipo kwa sasa na kwa wengi hilo ni la msingi pamoja  na kufuata kanuni za afya pia ni muhimu,” amesema.

Ligi Kuu Bara imesimamishwa kwa muda wa siku 30 ili kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vilianza kusambaa mwezi Desemba nchini China na Tanzania pia imeripotiwa kesi za wagonjwa zaidi ya watatu waliopata Corona.

HIKI NDICHO ANACHOKIFANYA MORRISON KUJILINDA NA CORONA NAMUNGO: TUTAREJEA KWENYE UBORA WA AWALI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply