Uncategorized

TAMBWE, NYOTA ALIYEWIKA YANGA ATAMANI KUREJEA TENA KUKINUKISHA

admin March 22, 2020 9:31 pm
 AMISSI Tambwe mshambuliaji wa zamani wa Yanga, amesema kuwa bado ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao, hivyo uongozi wa Yanga umpe dili ili asiani kandarasi mpya.
Tambwe aliwahi kutamba na klabu za Simba na Yanga, amesema anatamani kurudi Yanga kwa sababu ni timu ambayo anaipenda.
Kwa sasa Tambwe hana timu jambo linalompa nafasi ya kujiunga na klabu yoyote ambayo atafika nayo maelewena huku akisisitiza kuwa akipewa nafasi Yanga atatatua tatizo la ukame wa mabao.
“Bado nipo vizuri, sina mzaha nikiwa kwenye lango, Yanga wakinisajili nitawafanyia kazi kweli, unajua mimi nina mapenzi na Klabu ya Yanga, kwa hiyo nikirejea hapo nitaipambania kwa moyo wote,” amesema Tambwe.

Tambwe akiwa Bongo alifunga hattrick nne ambapo alifunga moja akiwa na Simba na tatu akiwa na Yanga zote ilikuwa Uwanja wa Taifa.
BALAA LA MZAMBIA ANAYEWINDWA NA SIMBA ACHA KABISA, DAU LAKE NOMA MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply