Uncategorized

NCHIMBI: PROGRAMU YA KOCHA MKUU ITANIRUDISHA KWENYE UBORA WANGU

admin March 23, 2020 5:04 pm

DITRAM Nchimbi, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa amepewa programu maalumu na Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael kwa kipindi hiki cha mapumziko.


Akizungumza na Saleh Jembe, Nchimbi amesema kuwa anatambua kwamba kiwango chake ni lazima kilindwe jambo linalomfaya afuate maelekezo ya Kocha Mkuu wa timu hiyo.

“Nimepewa programu maalumu ambayo nina amini itanifanya niwe bora na kuweza kurejea kwenye ubora ambao nilikuwa nao kikubwa ni kuamini na kutimiza yale ambayo ninaambiwa na kocha.

“Kwa sasa tunapita kipindi kigumu cha mpito ambapo ni lazima kila mmoja achukue tahadhari ya kujilinda na Virusi vya Corona,” amesema Nchimbi.

Kwenye Ligi Kuu Bara, Nchimbi ametupia mabao sita ambapo akiwa Yanga amefunga mabao mawili na kutoa asisti mbili na akiwa ndani ya Polisi Tanzania alifunga mabao manne.
AKILI ZA MBELGIJI WA YANGA EYMAEL ZIPO NAMNA HII NYOTA WA STARS ANASHINDA NDANI NCHINI MISRI KISA KORONA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply