Uncategorized

WATATU WAGUNDULIKA NA CORONA NDANI YA JUVENTUS, HALI BADO HAIJAWA SHWARI

admin March 23, 2020 4:04 am

MSHAMBULIAJI wa Juventus, Paulo Dybala anakuwa mchezaji wa tatu kugundulika na Virusi vya Corona ndani ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia, Serie A.
Nyota huyo mwenye miaka 26 amegundulika na Corona yeye pamoja na mpenzi wake  Oriana baada ya kupimwa.
Juventus imethibitisha kwamba nyota huyo alitengwa tangu Machi 11 ambapo alikuwa hajaonyesha dalili zozote za ugonjwa mpaka pale kipimo kilipothibitisha kwamba ameathirika kwani awali aligoma na kukanusha taarifa zilizoelzea kuwa ana Corona.
Wachezaji wengine ndani ya Juventus ambao wana Corona ni pamoja na Blaise Matuidi na Daniele Rugani.
Mchezaji wa kwanza ndani ya Serie A kugundulika na Corona alikuwa ni Rugani ambaye amekuwa akiwapa moyo wachezaji wengine kurejea kwenye morali na nguvu ya kuamini kwamba wanaweza kupona.
 Corona imekuwa tishio ambapo kwa upande wa michezo ligi zote zimesimamishwa na zinatarajia kurejea Aprili 30 iwapo hali itakuwa sawa.
YANGA YAINGIA ANGA ZA MZAWA HUYU KUWA MBADALA WA UBUTU WA SAFU YA USHAMBULIAJI SIMBA SASA WAANZA KUMVUTIA KASI NYOTA ANAYEKIPIGA MALAYSIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply