Uncategorized

YANGA YAINGIA ANGA ZA MZAWA HUYU KUWA MBADALA WA UBUTU WA SAFU YA USHAMBULIAJI

admin March 23, 2020 4:04 am

IMEELEZWA kuwa mshambuliaji mzawa namba moja ndani ya Namungo FC, Reliants Lusajo amewekwa kwenye rada na mabosi wa Yanga ili kuinasa saini yake kwa ajili ya kujiunga na kikosi hicho.

Lusajo ndani ya ligi ametupia mabao 11 na kutengeneza pasi nne za mabao ambapo anamfukizia kwa ukaribu mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere mwenye mabao 19 kwa kucheka na nyavu.

Habari zinaeleza kuwa Yanga imeweka hesabu za kumpata nyota huyo kuwa mbadala wa kutatua ubutu wa safu yao ya ushambuliaji ambayo kwa ujumla kwenye mechi 27 imefunga mabao 31 huku kinara wa kutupia akiwa ni David Molinga mwenye mabao nane.


Meneja wa Lusajo, Ahmad Kassim amesema kuwa suala la mchezaji wake kusepa ndani ya Namungo ni la muda tu kwani amebakiza kandarasi ya miezi mitatu jambo linalompa nafasi ya kuzungumza na timu yoyote.

“Kwa sasa Lusajo yupo huru kuzungumza na timu yoyote ana  mkataba wa miezi mitatu ndio umebaki kuhusu kwenda Yanga ni suala la kusubiri kwani mazungumzo bado hayajafanyika ila kipaumbele kikubwa ni kwa Namungo,” amesema.
KOCHA MTIBWA SUGAR: TAHADHARI YA CORONA NI LAZIMA IFUATWE NA WATU WOTE WATATU WAGUNDULIKA NA CORONA NDANI YA JUVENTUS, HALI BADO HAIJAWA SHWARI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply