Uncategorized

SALAMBA AJIFUNGIA NDANI AKIPIGA MATIZI KULINDA KIPAJI CHAKE

admin March 25, 2020 5:34 am


ADAM Salamba nyota wa Tanzania anayeperusha bendera ya Taifa nchini Kuwait amesema kuwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona kwa sasa anapiga matizi ndani ili kulinda kipaji chake.

Salamba ambaye ni mshambuliaji amepewa dili la kuitumikia timu ya Al Jahra akitokea Klabu ya Simba.

Akizungumza na Saleh Jembe, Salamba amesema kuwa kwa sasa hakuna ambaye anapata muda wa kufanya mazoezi pamoja na wachezaji wenzake kutokana na kusambaa kwa Corona.

“Hakuna ambaye anapata nafasi ya kufanya mazoezi pamoja na wachezaji wengine zaidi mimi mwenyewe ninafanya mazoezi nyumbani tena ndani ili kuendelea kulinda kipaji changu,” amesema.

HIVI NDIVYO MSUVA WA EL JADIDA ALIVYOFANYA KUCHUKUA TAHADHARI YA CORONA GADIEL MICHAEL: KUNA USHINDANI MKUBWA WA NAMBA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply