Uncategorized

PASCAL WAWA: TUCHUKUE TAHADHALI NA CORONA

admin April 2, 2020 1:44 am

BEKI kisiki wa Simba, Pascal Wawa, amesema kuwa Virusi vya Corona siyo vya kuchukulia utani, ni lazima kila mmoja achukue tahadhari.
Wawa amesema kuwa kwa sasa anafanyia mazoezi ndani kutokana na kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona.
“Nipo nyumbani na hali bado haijawa nzuri kwa sasa tunaomba Mungu mambo yarudi kama zamani kwani kwa sasa ninafanyia mazoezi nyumbani, hivyo ni lazima tuchukue tahadhari kuhusu Corona,” amesema Wawa.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo Serikali kupitia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ilitoa tamko hilo Machi 17.
VIDEO: BEKI POLISI TANZANIA ATAJA SIRI YA SAINI YAKE KUGOMBANIWA, AITAJA SIMBA MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTIXTRA ALHAMIS

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply