Uncategorized

ISHU YA BEKI WA COASTAL UNION KUIBUKIA SIMBA IPO NAMNA HII

admin April 4, 2020 9:02 pm
BAKARI Mwamnyeto, nahodha wa Coastal Union amesema kuwa hana hiyana iwapo kikosi cha Simba kitahitaji saini yake.

 Inaelezwa kuwa mabosi wa Simba wanahitaji huduma ya  beki huyo hali iliyofanya kumtengea dau la milioni 85.
Safu yake ya ulinzi imejijengea ukuta makini ambapo inashika nafasi ya pili kwa kuruhusu mabao machache ikiwa imefungwa 19 msimu huu na kinara akiwa ni Simba ambaye amefungwa mabao 15.
Beki huyo amesema:”Mimi ni mchezaji siwezi kuchagua timu ila kikubwa ni makubaliano na maslahi iwapo kila kitu kitakuwa sawa ninaweza kutumika ndani ya Simba hata nje ya Simba kwangu fresh,”.
HERITIER MAKAMBO AINGIA ANGA ZA YANGA TENA YANGA YAMVUTIA KASI NYOTA ANAYEKIPIGA NDANI YA CONGO, MAMBO NI MOTO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply