Uncategorized

MTIBWA SUGAR: MASHABIKI, WACHEZAJI WACHUKUE TAHADHARI YA CORONA

admin April 5, 2020 1:02 pm


THOBIAS Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa watanzania na mashabiki wanapaswa wachukue tahadhari ya Virusi vya Corona kwani ni janga la dunia nzima.

Kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona, Serikali ilizuia mikusanyiko isiyo ya lazima ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Bara.

Mtibwa Sugar ilivunja kambi yao Machi 17 na sasa wachezaji wapo nyumbani wakiendelea na mazoezi binafsi ambayo wamepewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kifaru amesema: :-“Tumewaambia wachezaji wetu wawe makini na kujilinda na Virusi vya Corona pia tunapenda kuwaomba mashabiki na watanzania kiujumla kuchukua tahadhari kujilinda na Virusi vya Corona,”.

AZAM FC: BADO HATUJAJUA HATMA YA LIGI ITAKUAJE TIMU TATU KUBWA ZAINGIA VITANI KUIWINDA SAINI YA MARIO GOTZE WA DORTMUND

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply