Uncategorized

NGASSA AJICHIMBIA MWANZA KWA SASA

admin April 7, 2020 9:40 am

MRISHO Ngassa, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kwa sasa amejichimbia Mwanza huku akichukua tahadhari ya kujilinda na Virusi vya Corona.

Ligi Kuu Tanzania Bara kwa sasa imesimamishwa kutokana na kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo wakati ligi inasimamishwa Yanga ilikuwa nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi 51 kibindoni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ngassa amesema kuwa yupo Mwanza akiendelea na ratiba zake na mpango wa kurudi Dar utakamilika hivi karibuni.

“Nipo Mwanza kwa sasa nikiendelea na ratiba zangu, mpango wa kurudi Dar utakuwa hivi karibuni, kikubwa ni kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Corona ili maisha yarudi kama zamani,” amesema.

CHESEA, NAPOLI ZAITAKA SAIN YA CAVAN KLABU TUNISIA YAMTUMIA MWALIKO MOLINGA ..YEYE AMEJIBU HAYA!!

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply