Uncategorized

MBAO FC YAGOMA KUSHUKA DARAJA

admin April 8, 2020 5:03 am


WAZIR Jr, mshambuliaji wa Mbao FC amesema kuwa anaimani kuwa timu yao haitashuka daraja kutokana na mipango ambayo itapangwa baada ya ligi kurejea.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Wazir amesema kuwa mipango mikubwa ni kuona timu inapata matokeo chanya kwenye mechi zilizobaki jambo litakalowabakiza kwenye ligi.

“Bado tuna nafasi ya kubaki ndani ya ligi kutokana na mipango ambayo tutakuja nayo pindi ligi itakaporejea, imani yangu tutakuwa vizuri na tutapambana kupata matokeo,” amesema.

Mbao FC ipo nafasi ya 19 ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi 28.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA BETIKA, BURE KABISA MO RASHID: MUHIMU KUCHUKUA TAHADHARI YA VIRUSI VYA CORONA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply