Uncategorized

KISA CHAMA, SIMBA KUISHTAKI YANGA

admin April 14, 2020 6:27 am

UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo kwenye mpango wa kuwashtaki Yanga kutokana na suala lao la kutaka kuipata saini ya nyota wao Clataos Chama raia wa Zambia.

Yanga imeripotiwa kuwa kuanza kufanya mazungumzo na Chama ambaye ni mali ya Simba jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kwa kuwa Simba inaeleza kuwa ana mkataba mrefu ndani ya Simba.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa ni lazima kanuni zifuatwe na kusimamiwa hivyo kwa kosa lao la kufanya mazungumzo na Chama watawashtaki.

“Kanuni za mpira zipo wazi na jambo ambalo linazungumzwa ni kinyume na utaratibu uliopo ni lazima tufanye jambo ili kuwafunnza Yanga katika hili, ipo wazi kabisa,” amesema.

Chanzo: Wasafi

MABOSI WA YANGA WAPANIA KUWA NA KIKOSI MATATA AFRIKA MASHARIKI NA KATI LIVERPOOL YAHAHA KUMPATA MBADALA WA MANE IWAPO ATASEPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply