Uncategorized

JAMES KOTEI ATAJA SABABU ZITAKAZOMRUDISHA SIMBA

admin April 16, 2020 2:01 pm

JAMES Kotei, kiungo mkabaji ambaye alicheza kwa mafanikio ndani ya Klabu ya wa Simba amesema kuwa anapenda kurudi ndani ya Simba kwa kuwa hakuzinguana na viongozi wakati akicheza msimu uliopita kabla ya kutimka jumla.

Kocha wa wakati huo aliyekuwa naye Kotei ndani ya Simba Patrick Aussems alisema kuwa alikuwa anahitaji huduma ya Kotei ila mambo yalikuwa magumu kwani ilishindakana kubaki.

“Miongoni mwa wachezaji ambao nilikuwa nahitaji kupata huduma yao alikuwa ni Kotei ila ninadhani uongozi ulimpa ruhusa kuondoka katika hilo siwezi kuingilia,” alisema Aussems kabla ya kuchimbishwa.

Kotei ambaye baada ya kutimka Simba alikipiga Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na kwa sasa yupo ndani ya Belarus amesema: “Uzuri ni kwamba viongozi wa Simba pamoja na wachezaji wote ni familia, ninapenda kuwa sehemu ambayo ninakuwa na furaha sioni shida kurudi tena iwapo mambo yatakuwa safi.

“Kazi ya mchezaji ni kucheza hilo lipo wazi nami pia ni mchezaji popote kwangu nakipiga,”.

MWAMNYETO, NYOTA ANAYEWINDWA NA SIMBA NA YANGA ATOA YA MOYONI FUNDI WA KUCHEKA NA NYAVU ATOA TAMBO ZA KUTOSHA KABLA YA KUTUA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply