Uncategorized

KEVIN DE BRUYNE AJIPA UBALOZI WA HIYARI

admin April 17, 2020 9:01 am

KIUNGO mtengeneza mipango ndani ya Klabu ya Manchester City, Kevin De Bruyne amesema kuwa amekuwa balozi mzuri kwa sasa kwenye familia yake kuhusu kujilinda na Virusi vya Corona.
Kiungo huyo anayekipiga timu ya Taifa ya Ubelgji amesema kuwa mwanzo familia yake ilikuwa na hofu kubwa kuhusu maambukizi hayo jambo lililomfanya awe balozi mzuri kuhusu maambukizi ya Virusi vya Corona.
Nyota huyo kwa msimu wa 2019/20 ametupia jumla ya mabao nane na kutoa pasi 16 za mabao akiwa ni kinara kwa kutengeneza pasi za mwisho msimu huu.
Kwa sasa Ligi Kuu England imesimamishwa na inatarajiwa kurejea Aprili 30 huku klabu zikihitaji Ligi Kuu England imalizike Juni 30.
“Kulikuwa na hofu kwa familia yangu mwanzo jambo ambalo lilinifanya niweze kuzungumza na mke wangu pamoja na watoto kuhusu kujilinda kuwa salama na maambukizi haya ya Virusi vya Corona, ninajua kwa mashabiki pia hali yao ni ya huzuni kutokana na kupenda mpira lakini afya ni muhimu zaidi,” amesema.
HATMA YA NYOTA WA ZAMANI WA YANGA IPO KWA MROMANIA WA AZAM FC KOCHA REAL MADRID ATOA MSAADA AFRIKA KWA AJILI YA KUPAMBANA NA VIRUSI VYA CORONA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply