Uncategorized

KUHUSU USAJILI WA WACHEZAJI WANAOKIPIGA NDANI YA BONGO SIMBA YASEMA HAISHINDWI KUSAJILI

admin April 17, 2020 3:31 pm

SENZO Mazingisa,Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba amesema kuwa timu yake haishindwi kumsajili mchezaji yeyote anayecheza katika ligi ya Tanzania ikiwa inamhitaji.

Simba imekuwa ikihusishwa na usajili wa baadhi ya wachezaji wanaocheza Ligi Kuu Bara kama beki wa Coastal Union, Bakari Mwamnyeto, beki wa Azam FC, Yakubu Mohammed na kiungo wa Polisi Tanzania, Baraka Majogoro. 

Senzo amesema kuwa kutokana na aina ya wachezaji wanaopatikana hapa nchini, timu hiyo haishindwi kumsajili mchezaji yeyote ambaye watakuwa wakimhitaji labda kama hawana mpango na mchezaji huyo.


“Ikiwa tunahitaji kupata saini ya mchezaji ndani ya Ligi Kuu Bara Tanzania hatuwezi kushindwa labda tuwe hatuna mpango naye,” amesema.

KOCHA WA SIMBA ASEPA NA MTU, KESHO NDANI YA GAZETI LACHAMPIONI JUMAMOSI KUPAMBANA NA VIRUSI VYA CORONA NI MUHIMU, ILA WACHEZAJI MSIPUUZIE PROGRAM ZENU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply