Uncategorized

MWAMBA WA LUSAKA CHAMA ATAJA MASHARTI YA KUTUA YANGA

admin April 19, 2020 7:29 am

CLATOUS Chama, nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Simba amesema kuwa Yanga haiwezi kuipata saini yake msimu ujao wa mwaka 2020/21 kutokana na kuwa mali ya Simba labda msimu unaofuata wa mwaka 2021/22.

Chama amekuwa kwenye sarakasi za usajili msimu huu ambapo Yanga ilielezwa kuwa inaitaka saini yake jambo lililowafanya Simba kupelekea malalamiko Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kile walichoeleza kuwa Yanga wamekiuka utaratibu wa usajili.

Akizungumzia ishu ya kutua Yanga Chama amesema:”Kuhusu kuhitajika na Yanga ni jambo zuri ila kwa msimu ujao haitawezekana labda ule unaofuata inawezekana.

“Lakini yote yatakuwa sawa ikiwa utaratibu wa usajili utafuata na makubaliano yakawa sawa,” amesema.

Mkataba wa Chama unameguka mwaka 2021 aliongeza mkataba wa miaka miwili msimu wa 2018/19.

SENZO – TULIENI..MAMBO MAZURI YANAKUJA MSIMBAZI HUMUD ACHEKELEA DILI LA KUJIUMGA NA YANGA, AZUNGUMIZA MAISHA YAKE NDANI YA MTIBWA SUGAR

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply