Uncategorized

SAKATA LA CHAMA KUTUA JANGWANI..MWAKALEBELA ATAKIWA KUJIUZULU YANGA

admin April 19, 2020 4:18 pm

MCHEKESHAJI mkongwe Bongo, Steven Mangele (Steve Nyerere), amemtaka Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Frederick Mwakalebela kuachia ngazi katika nafasi hiyo ili kulinda heshima yake kufuatia sakata la usajili wa kiungo wa Simba, Clatous Chama kufika kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mwakalebela aliutibua uongozi wa Klabu ya Simba mara baada ya kudai kuwa amefanya mazungumzo na Chama wakitaka kumsajili, huku akijua kuwa nyota huyo yupo katika mkataba na timu yake, kitendo kilichosababisha uongozi wa Simba kupeleka barua ya malalamiko TFF.

Licha ya kuwa Mwakalebela aliomba msamaha na kudai kuwa alikuwa anafanya utani kama ambavyo Simba walifanya kwa nahodha wao, Papy Tshishimbi, haikuweza kuwa msaada kwa wakati huo na Simba wakaenda mbele zaidi kama walivyoahidi.

 Kupitia ukurasa wake wa Instagram Steve aliweka ujumbe uliosomeka kuwa: “Unapokuwa umechaguliwa na wapiga kura, wakiamini tunachagua mtu makini, na mwenye kauli zilizonyooka kwa maslahi ya Yanga.

 “Ikatokea ukapindisha yale yaliyotarajiwa na wapiga kura wako, basi una kazi moja ya kujiuzulu, nadhani kuna haja ya kuachia ngazi kwa kulinda heshima yako uliyoijenga kwa muda mrefu, moja ya sifa ya kuwajibika ni kutunza heshima yako. Bro nakushauri ujiuzulu.”

KUNA STRAIKA WA BURUNDI ANAITAKA YANGA, KESHO NDANI YA CHAMPIONI JUMATATU YANGA YA GSM YAZIDI KUNOGA…KUINGIA MKATABA NA KLABU KIGOGO YA HISPANIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply