Uncategorized

YANGA YAINGIA ANGA ZA RASTA HUYU WA MTIBWA SUGAR

admin April 24, 2020 6:35 am

SALUM Kihimbwa, mshambuliaji wa Mtibwa Sugar mwenye rasta kichwani ameingia kwenye hesabu za mabosi wa Yanga ambao wanahitaji kuboresha kikosi chao msimu ujao.
Hivi karibuni Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa walikuwa na skauti ya kufuatilia wachezaji wa ndani kwa ukaribu ili kujua nani atawafaa pale dirisha la usajili litakapoanza ambapo habari zinaeleza kuwa Mtibwa Sugar rasta Kihimbwa ni miongoni mwao.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru alisema kuwa anatambua kuwa timu nyingi zinasaka wachezaji wao kutokana na ubora wao jambo ambalo haliwapi mashaka.
“Sio Yanga tu hata Simba, Azam na timu nyingine zimekuwa zikiitazama wachezaji wa Mtibwa Sugar ili kuwapata hilo lipo wazi, wanakwenda wanarudi tunawanoa tena si unamuona Hassan Dilunga alisajiliwa akaachwa ila aliporudi tumemrudisha kwenye ubora na sasa matunda yake yanaonekana.
“Iwapo wanahitaji kusajili kwa sasa hapana kuna mambo ya kitaifa tunayafanya ambayo ni kupambana dhidi ya Corona haya yakiisha tutakaa mezani tujadili,” alisema Kifaru.
SABABU ZA UWANJA WA AZAM COMPLEX KUWA SAWA NA TP MAZEMBE HIZI HAPA OBREY CHIRWA ATOA NENO LA KISHUJAA AZAM FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply