Uncategorized

DIAMOND KUCHANGIA KODI YA PANGO KAYA 500 NCHINI

admin April 25, 2020 3:02 pm



MWANAMUZIKI Nasibu Abdul, ‘Diamond Platinumz’ amesema kuwa atachangia ‘kodi ya pango’ kwa kaya 500 nchini kwa ajili ya kupunguza makali ya kiuchumi wakati huu ambapo Watanzania wanapambana dhidi ya virusi vya Corona.


Diamond amesema:”Najua katika kipindi hiki cha Corona, mambo mengi hayajakaa sawa, hususani upande wa biashara nyingi zimeshuka na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa kidogo magumu kwa wengi wetu na mimi ni miongoni mwa walio ndani ya janga hili. 

Amesema kupitia ukurasa wake wa  Instagram nyota huyo ameeleza kuwa taarifa na utaratibu zaidi utatangazwa siku ya Jumatatu juu ya namna kaya hizo 500 zitakavyopatikana na kuweza kupata msaada huo.

Diamond Platnumz anakuwa msanii wa kwanza nchini kujitokeza hadharani na kuweka bayana kuwa atasaidia chochote wakati huu wa janga la mlipuko wa Virusi vya Corona vyenye kusababisha homa kali ya mapafu yaani Corona.

TANZIA: KOCHA BONGO AFARIKI UNAAMBIWA KELVIN YONDANI ANATISHA BALAA,KESHO NDANI YA SPOTIXTRA JUMAPILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply