Uncategorized

BALAA LA KIUNGO ANAYEWINDWA NA YANGA NI ZAIDI YA MORRISON

admin May 4, 2020 9:47 pm


ALLY Niyonzima, kiungo anayekipiga ndani ya Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda inaelezwa kuwa ni hatari ndani ya uwanja zaidi ya Bernard Morrison ambaye kwa sasa ndiye nyota namba moja.

Inaelezwa kuwa Yanga ipo kwenye mchakato wa kuisaka saini ya Niyonzima ili kuongeza makali ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya msimu wa 2020/21.

Clever Kazungu, Ofisa Habari wa APR ya Rwanda ambao ni washindani wakubwa wa Klabu ya Rayon Sports anayocheza Niyonzima amesema kuwa ni miongoni mwa wachezaji wazuri na hatari ndani ya uwanja.

“Ni miongoni mwa wachezaji ambao wana uwezo mkubwa ndani ya uwanja na endapo atatua Bongo itakuwa ni habari nyingine kwani ana uwezo mkubwa wa kufanya mambo mengi uwanjani huku akiisaidia timu kupata matokeo.

“Ana uwezo wa kukaba, kufunga na kutengeneza mashambulizi pia ana uwezo wa kuchezea mpira vile vitu vinavyofanywa na Morrison kuupanda mpira yeye anaweza pia kufanya hivyo na madoido mengine,” amesema. 

NYOTA SIMBA APATA OFA YA KUKIPIGA NCHINI ETHIOPIA MTAZAMO WA SALEH JEMBE KUHUSU SIMBA NA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply