Uncategorized

SERIKALI YAITAKA TFF KUPIGA HODI FIFA KUHUSU LIGI

admin May 5, 2020 4:58 pm

WAZIRI wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema kuwa kuna umuhimu wa Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kufanya mazungumzo na Fifa ili kujua namna gani wanaweza kumaliza ligi kwa wakati.

Mwakyembe amesema kuwa kuna umuhimu wa TFF kukaa pamoja na Fifa ili kuona namna bora itakayowafanya wamalize ligi bila kuwaumiza wachezaji.

“Wakati ule ligi ilipokuwa ikiendelea hali ilipokuwa shwari bila ya uwepo wa Virusi vya Corona kulikuwa na ratiba ngumu kwa timu jambo ambalo tulikuwa tunawashauri TFF kulitazama kwa umakini.

“Unakuta kuna timu ina mchezo Mbeya ikitoka hapo inakwenda Iringa yaani hakukuwa na muda wa timu kupumzika ila kwa sasa kuna umuhimu wa kulitazama hili kwa umakini.

“Rais amesema kuwa anafikiria kuirejesha ligi lakini tutakapoitwa lazima tuwe na mrejesho mzuri wa kuzungumza naye ili apate kutupa ruhusa ya kuendelea na ligi,” amesema.

ARUSHA FC YAIANGUKIA TFF NA WADAU, HALI NI TETE KOCHA WA YANGA AKWAMA UBELGIJI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply