Uncategorized

KIUNGO YANGA AOMBA MKATABA SIMBA

admin May 6, 2020 1:56 pm


KIUNGO wa zamani wa Yanga, Mbrazil, Andrey Coutinho, ameibuka na kuwaambia viongozi wa Simba kuwa yupo tayari kurejea nchini kujiunga na timu hiyo.


Coutinho anayekipiga katika klabu ya Ayutthaya United ya nchini Thailand, aliwahi kuchezea Yanga katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2016, akitokea Taubate SP ya kwao Brazil. 

Coutinho amesema kuwa bado anatamani kuona anapata nafasi nyingine ya kucheza Ligi ya Tanzania akiwa na timu yoyote ikiwemo Simba kama watakuwa tayari kumpa mkataba.


“Sasa hivi nacheza Thailand, lakini bado naikumbuka sana Tanzania kwa sababu ilikuwa nchi yangu ya kwanza kucheza soka la kulipwa, natamani kuona narudi tena kucheza katika timu yoyote, lakini zaidi Simba,” amesema.

HESABU ZA KAGERA SUGAR ZIPO NAMNA HII, CORONA ILITIBUA MAMBO KAGERE AMEKUMBUKA MPIRA, CORONA YAMFANYA ASHINDE NDANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply