Uncategorized

NYOTA SIMBA AKUBALI KUTUA YANGA

admin May 12, 2020 9:21 pm


KIUNGO Mohammed  Ibrahim, ‘Mo’ amesema kuwa yupo tayari kujiunga na Yanga kwenye msimu ujao kama wakihitaji saini yake.

Nyota huyo anakipiga kwa mkopo Namungo FC ya Lindi akitokea Simba, ni kati ya wachezaji ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
  
Mo amesema kuwa tayari baadhi ya klabu zimemfuata ikiwa ni pamoja na Namungo kumpa ofa ambazo zipo kwenye majadiliano ya dau la usajili ambalo yeye analitaka ili asaini.
“Mkataba wangu na Simba unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, na kama mambo yakienda vizuri basi nitaondoka hapo na kwenda kwingine kutafuta changamoto mpya.
“Tayari baadhi ya klabu zimenifuata kwa ajili ya kufanya mazungumzo na kikubwa kujadiliana katika dau la usajili ambalo mimi ninalitaka, ni mapema kuzitaja klabu hizo, tusubirie muda muafaka ukifika itaweka wazi.
“Kikubwa nimepanga kufanya mengi makubwa katika msimu ujao kwenye klabu hiyo mpya nitakayokwenda kuichezea, hakuna asiyefahamu kiwango change, hivi sasa ninafanya mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kujiweka fiti zaidi,” alisema Mo. 

Mo aliyewahi kuichezea timu ya taifa, Taifa Stars, alijiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar.
KUMBE MAJUNGU YALIMUONDOA NDANI YA YANGA TAMBWE MILIONI 800 ZAFUMUA KIKOSI SIMBA NDANI YA GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply