Uncategorized

MTAMBO WA MABAO NDANI YA SIMBA WAMKOSHA SVEN, SASA KAZI IPO

admin May 19, 2020 11:47 am


MIRAJ Athuman, ‘Sheva’ kiungo mshambuliaji ndani ya Klabu ya Simba amemkosha Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ambaye amesema kuwa ana imani msimu ujao atafanya mambo makubwa.

Sheva msimu huu kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa alitumia dakika 508 uwanjani kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Kwa sasa tayari Sheva ameanza kurejea kwenye ubora wake na ameanza mazoezi ya kucheza mpira pamoja na yale ya viungo.

Sven amesema:” Miraj yupo Kwenye hesabu zangu na ninaamini akirejea atakuwa bora hivyo ni jambo la kusubiri na kuona itakuaje.” 


Sheva ametupia mabao sita na kutengeneza pasi moja ya bao lilikutana na Meddie Kagere.

KILICHOMZUIA MOLINGA KUSEPA BONGO HIKI HAPA DILI LA SIMBA NA MSHAMBULIAJI MGHANA WA ASANTE KOTOKO LIMEISHA KWA MTINDO HUU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply