Uncategorized

HESABU ZA YANGA NI KUSEPA NA UBINGWA MSIMU WA 2019/20

admin May 25, 2020 7:47 am
UONGOZI wa Yanga umesema kuwa una imani ya kufanya maajabu pale Ligi Kuu Bara itakaporejea Juni Mosi kwa wachezaji wao kujituma kupata matokeo ili kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa kama ilivyo kwa wapinzani wao Simba ambao ni mabingwa watetezi.
Ligi kuu wakati inasimamishwa, Yanga ilikuwa na pointi 51 ikiwa imecheza mechi 27 ikiachwa kwa pointi 20 na vinara Simba ambao wamecheza mechi 28.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji na Msemaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kurejea kwa ligi kunamaanisha kwamba ile burudani ambayo walianza kuitoa inarejea.
β€œBurudani inarejea tuliikosa kwa muda mrefu, tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zetu zilizobaki hivyo tukichanga karata zetu tunaweza kutwaa ubingwa wa ligi pamoja na lile la Kombe la Shirikisho.
β€œKila kitu kinawezekana kikubwa ni mashabiki kutupa sapoti na kuendelea kuwa nasi bega kwa bega, wachezaji wetu wanaari kubwa na nguvu ukizingatia kwamba walikuwa wanaendelea na mazoezi,watakapowasili kambini mipango yote itapangwa,” amesema Nugaz.
CHAMA ANACHEKELEA AKITOKEA UPANDE WA KUSHOTO JEMBE LA KAZI LA SIMBA LINALOTUA LEO ACHA KABISA, LINAFUNGA NA KUTOA PASI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply