Uncategorized

MBARAKA YUSUPH AREJEA MZIGONI

admin May 28, 2020 7:47 am


MBARAKA Yusuph, mshambuliaji wa Azam FC amesema kuwa kwa sasa yupo vizuri kuendelea kupambana kwenye mechi za ushindani.

Mbaraka alikuwa nje akitibu majeraha yake aliyopata wakati akiwa ndani ya Klabu ya Namungo kwa mkopo msimu uliopita kwa sasa ameshaanza mazoezi na wachezaji wenzake.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mbaraka amesema kuwa wakati wa mapumziko ya ligi yaliyotokana na janga la Virusi vya Corona alikuwa anafanya mazoezi binafsi na sasa yupo kambini.

“Nilikuwa ninafanya mazoezi binafsi nilipokuwa nyumbani na sasa tayari ninaendelea vizuri nikiwa kambini na wachezaji wenzangu, kikubwa ni kuendelea kupambana na kumuomba Mungu ili tuzidi kuwa salama,” amesema.

MKWASA ASHIKILIA MIKOBA YA MBELGIJI WA YANGA VILIO INATOSHA, MALIZENI MSIMU MAISHA YAENDELELEE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply