Uncategorized

YANGA YAOMBA SAPOTI YA MASHABIKI

admin June 5, 2020 11:47 am


PAPY Tshishimbi, nahodha wa Yanga amesema kuwa kikubwa ambacho kinahitajika kwa sasa kutoka kwa mashabiki ni sapoti yao mwanzo mwisho.

Tshishimbi amesema kuwa ni jambo la msingi kwa mashabiki kuendelea kuipa sapoti timu yao kwa kuwa inarejea ikiwa katika ubora wa kipekee.

“Wachezaji licha ya kwamba walikuwa nyumbani bado walikuwa wanafanya mazoezi hivyo kinachotakiwa kwa sasa ni mwendelezo wa sapoti ya mashabiki ambayo ilikuwa ipo tangu zamani.

“Kwa sasa kuna jambo la msingi ambalo tunalifanya ni kuendelea kufanya mazoezi kwa wachezaji waliofiti huku mimi nikiwa naskilizia nirejee kwenye ubora wangu kwani niliumia mazoezini ila ninaendelea vizuri,” amesema Tshishimbi.

Jumapili, Yanga itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC ikiwa ni mchezo wa kupima maendeleo ya wachezaji Uwanja wa Uhuru.

SVEN: WACHEZAJI WAPO VIZURI, BADO TUNAENDELEA KUWAREJESHA KWENYE UBORA AZAM FC KUKIWASHA KESHO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply