Uncategorized

HIVI NDIVYO POGBA ATAKAVYOCHEZA KIKOSI CHA KWANZA NA BRUNO

admin June 11, 2020 4:47 am


OLE Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amepanga kumtumia jumlajumla kiungo wake Paul Pogba sambamba na Bruno Fernandes kiungo mpya ambaye aliletwa ndani ya United kuwa mbadala wa Pogba ambaye alikuwa majeruhi.

Pogba atatumika akiwa ni kama namba 10 huku Fernandes akiwa ni kama kiungo mchezeshaji.

Inaelezwa kuwa Pogba kwenye mazoezi amekuwa akichezeshwa kama namba 10 pembeni ya straika na amekuwa akifanya vizuri.

Fernandes amekuwa bora ndani ya United tangu atue kikosini hapo Januari akitokea Klabu ya Sporting na amekuwa ni mchezaji wa kutegemewa akiwa amecheza mechi 5 na kufunga mabao mawili ndani ya United.

VIDEO:TAZAMA MABAO YA AZAM FC NA KMC,MCHEZO WA KIRAFIKI MANAHODHA WAKIUZIANA VIBANDA VIDEO: MBELGIJI AZUNGUMZIA HATMA YA MOLINGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply