Uncategorized

REAL MADRID,CHELSEA ZAKUTANA KWA KIUNGO KAI

admin June 11, 2020 9:47 am


KAI Havertz, kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Bayer Leverkusen anatajwa kuwindwa na Klabu ya Real Madrid iliyo chini ya Kocha Mkuu, Zinadine Zidane.

Inaelezwa kuwa Madrid itapata ushindani mkubwa kutoka kwa Chelsea iliyo chini ya Kocha Mkuu, Frank Lampard ambaye naye pia anatajwa kuiwinda saini ya nyota huyo.

Lampard bado anafikiria kumpata Timo Werner kutoka RB Leipzig jambo hilo linampa matumaini ya kupata saini ya nyota huyo Havertz ili kuunganisha pacha mpya msimu ujao.

Sababu kubwa ya kiungo huyo mwenye miaka 21 saini yake kuwaniwa ni pamoja na uwezo wake wa kucheza akiwa winga pamoja na kujua kufunga mabao jambo linalofanya timu zote mbili kuwa tayari kupata saini yake kwa mujibu wa The Sun.

YANGA: TUPO TAYARI KUIVAA MWADUI FC, WAMSHUKURU MUNGU KUWALINDA VIDEO: BAADA YA KUWATUNGUA SIMBA NA YANGA, MTUPIAJI ILANFYA AWEKWA KWENYE RADA ZAO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply